The Noble Qur'an Encyclopedia
Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languagesThe Opening [Al-Fatiha] - Swahili translation - Ali Muhsen Al-Berwani
Surah The Opening [Al-Fatiha] Ayah 7 Location Maccah Number 1
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU . [1]
Sifa njema zote ni za Mwenyeezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote; [2]
Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu; [3]
Mwenye kumiliki siku ya malipo. [4]
Wewe tu tunakuabudu, na wewe tu tunakuomba msaada. [5]
Tuongoe njia iliyonyooka. [6]
Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa, wala walio potea. [7]