The Noble Qur'an Encyclopedia
Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languagesThe Chargers [Al-Adiyat] - Swahili translation - Ali Muhsen Al-Berwani
Surah The Chargers [Al-Adiyat] Ayah 11 Location Maccah Number 100
Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua, [1]
Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini, [2]
Wakishambulia wakati wa asubuhi, [3]
Huku wakitimua vumbi, [4]
Na wakijitoma kati ya kundi, [5]
Hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi! [6]
Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo! [7]
Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali! [8]
Kwani hajui watakapo fufuliwa waliomo makaburini? [9]
Na yakakusanywa yaliomo vifuani? [10]
Kuwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na khabari zao wote! [11]