The Noble Qur'an Encyclopedia
Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languagesThe Elephant [Al-fil] - Swahili translation - Ali Muhsen Al-Berwani
Surah The Elephant [Al-fil] Ayah 5 Location Maccah Number 105
Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo watenda wale wenye tembo? [1]
Kwani hakujaalia vitimbi vyao kuharibika? [2]
Na akawapelekea ndege makundi kwa makundi, [3]
Wakiwatupia mawe ya udongo wa Motoni, [4]
Akawafanya kama majani yaliyo liwa! [5]