The Noble Qur'an Encyclopedia
Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languagesAlms Giving [Al-Maun] - Swahili translation - Ali Muhsen Al-Berwani
Surah Alms Giving [Al-Maun] Ayah 7 Location Maccah Number 107
Je! Umemwona anaye kadhibisha Malipo? [1]
Huyo ndiye anaye msukuma yatima, [2]
Wala hahimizi kumlisha masikini. [3]
Basi, ole wao wanao swali, [4]
Ambao wanapuuza Sala zao; [5]
Ambao wanajionyesha, [6]
Nao huku wanazuia msaada. [7]