The Noble Qur'an Encyclopedia
Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languagesThe day break [Al-Falaq] - Swahili translation - Ali Muhsen Al-Berwani
Surah The day break [Al-Falaq] Ayah 5 Location Maccah Number 113
Sema: Najikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko, [1]
Na shari ya alivyo viumba, [2]
Na shari ya giza la usiku liingiapo, [3]
Na shari ya wanao pulizia mafundoni, [4]
Na shari ya hasidi anapo husudu. [5]