The Noble Qur'an Encyclopedia
Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languagesThe mankind [An-Nas] - Swahili translation - Ali Muhsen Al-Berwani
Surah The mankind [An-Nas] Ayah 6 Location Maccah Number 114
Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa wanaadamu, [1]
Mfalme wa wanaadamu, [2]
Mungu wa wanaadamu, [3]
Na shari ya wasiwasi wa Shetani, Khannas, [4]
Anaye tia wasiwasi katika vifua vya watu, [5]
Kutokana na majini na wanaadamu. [6]