عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

The Believers [Al-Mumenoon] - Swahili translation - Ali Muhsen Al-Berwani

Surah The Believers [Al-Mumenoon] Ayah 118 Location Maccah Number 23

Kisha tukamjaalia awe tone ya mbegu ya uzazi katika kalio madhubuti. [13]

Akasema (Nuhu): Mola wangu Mlezi! Ninusuru kwa kuwa wamenikanusha. [26]

Na sema: Mola wangu Mlezi! Niteremshe mteremsho wenye baraka, na Wewe ni Mbora wa wateremshaji. [29]

Hakika katika hayo yapo mazingatio. Na kwa yakini Sisi ni wenye kuwafanyia mtihani. [30]

Akasema: Mola wangu Mlezi! Ninusuru kwa sababu wananikanusha. [39]

(Mwenyezi Mungu) akasema: Baada ya muda mchache watakuwa wenye kujuta. [40]

Basi wakawakanusha, na wakawa miongoni mwa walio angamizwa. [48]

Na tukamfanya mwana wa Mariamu na mama yake kuwa ni Ishara, na tukawapa makimbilio kwenda mahali palipo inuka penye utulivu na chemchem za maji. [50]

Basi wote hao ndio wanao kimbilia katika mambo ya kheri, na ndio watakao tangulia kuyafikia. [61]

Hata tutakapo watia katika adhabu wale walio dekezwa kwa starehe kati yao, hapo ndipo watapo yayatika. [64]

Na huku mkitakabari na usiku mkiizungumza (Qur'ani) kwa dharau. [67]

Na lau tungeli warehemu na tukawaondolea shida waliyo nayo bila ya shaka wangeli endelea katika upotofu wao vile vile, wakitangatanga. [75]

Watasema: Ni vya Mwenyezi Mungu! Sema: Basi, je, hamkumbuki? [85]

Watasema: Ni vya Mwenyezi Mungu. Sema: Basi je, hamwogopi? [87]

Watasema: (Ufalme huo) ni wa Mwenyezi Mungu. Sema: Basi vipi mnadanganyika? [89]

Sema: Mola wangu Mlezi! Ukinionyesha adhabu waliyo ahidiwa, [93]

Na sema: Mola wangu Mlezi! Najikinga kwako na wasiwasi wa mashet'ani. [97]

Na najikinga kwako, Mola wangu Mlezi, wasinikaribie. [98]

Mola wetu Mlezi! Tutoe humu Motoni. Na tufanyapo tena basi kweli sisi ni wenye kudhulumu. [107]

Atasema Mwenyezi Mungu: Tokomeeni humo, wala msinisemeze. [108]

Nawe sema: Mola wangu Mlezi! Samehe na urehemu nawe ni Mbora wa wanao rehemu. [118]