The Noble Qur'an Encyclopedia
Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languagesThose who set the ranks [As-Saaffat] - Swahili translation - Ali Muhsen Al-Berwani
Surah Those who set the ranks [As-Saaffat] Ayah 182 Location Maccah Number 37
Naapa kwa wanao jipanga kwa safu. [1]
Na kwa wenye kukataza mabaya. [2]
Na kwa wenye kusoma Ukumbusho. [3]
Hakika Mungu wenu bila ya shaka ni Mmoja. [4]
Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na yaliyomo kati yao, na ni Mola Mlezi wa mashariki zote. [5]
Hakika Sisi tumeipamba mbingu ya karibu kwa pambo la nyota. [6]
Na kulinda na kila shet'ani a'si. [7]
Wasiweze kuwasikiliza viumbe watukufu. Na wanafukuzwa huko kila upande. [8]
Wakifurushwa. Na wanayo adhabu ya kudumu. [9]
Isipo kuwa anaye nyakua kitu kidogo, na mara humfwatia kimondo kinacho ng'ara. [10]
Hebu waulize: Je! Wao ni wenye umbo gumu zaidi au hao wengine tulio waumba. Hakika Sisi tuliwaumba wao kwa udongo unao nata. [11]
Bali unastaajabu, na wao wanafanya maskhara. [12]
Na wanapo kumbushwa hawakumbuki. [13]
Na wanapo ona Ishara, wanafanya maskhara. [14]
Na husema: Haya si chochote ila ni uchawi tu ulio dhaahiri. [15]
Ati tukisha kufa na tukawa udongo na mifupa ndio kweli tutafufuliwa? [16]
Hata baba zetu wa zamani? [17]
Sema: Naam! Hali nanyi ni madhalili. [18]
Huko utapigwa ukelele mmoja tu! Na hapo ndio wataona! [19]
Watasema: Ole wetu! Hii ndiyo Siku ya Malipo. [20]
Hii ndiyo Siku ya Hukumu mliyo kuwa mkiikadhibisha. [21]
Wakusanyeni walio dhulumu, na wake zao, na hao walio kuwa wakiwaabudu. [22]
Badala ya Mwenyezi Mungu. Waongozeni njia ya Jahannamu! [23]
Na wasimamisheni. Hakika hao watasailiwa: [24]
Mna nini? Mbona hamsaidiani? [25]
Bali hii leo, watasalimu amri. [26]
Watakabiliana wao kwa wao kuulizana. [27]
Watasema: Kwa hakika nyinyi mlikuwa mkitujia upande wa kulia. [28]
Watasema (wakubwa): Bali nyinyi wenyewe hamkuwa Waumini. [29]
Sisi hatukuwa na mamlaka juu yenu, bali nyinyi wenyewe mlikuwa wapotovu. [30]
Basi hukumu ya Mola wetu Mlezi imekwisha tuthibitikia. Hakika bila ya shaka tutaonja tu adhabu. [31]
Tulikupotezeni kwa sababu sisi wenyewe tulikuwa wapotovu. [32]
Basi wao kwa hakika siku hiyo watashirikiana katika adhabu pamoja. [33]
Hivyo ndivyo tutakavyo wafanyia wakosefu. [34]
Wao walipo kuwa wakiambiwa La ilaha illa 'Llahu Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu tu, wakijivuna. [35]
Na wakisema: Hivyo sisi tuiache miungu yetu kwa ajili ya huyu mtunga mashairi mwendawazimu? [36]
Bali huyu amekuja kwa Haki, na amewasadikisha Mitume. [37]
Hakika nyinyi bila ya shaka mtaionja adhabu chungu. [38]
Wala hamlipwi ila hayo mliyo kuwa mkiyafanya. [39]
Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio khitariwa. [40]
Hao ndio watakao pata riziki maalumu, [41]
Matunda, nao watahishimiwa. [42]
Katika Bustani za neema. [43]
Wako juu ya viti wamekabiliana. [44]
Wanazungushiwa kikombe chenye kinywaji cha chemchem. [45]
Kinywaji cheupe, kitamu kwa wanywao. [46]
Hakina madhara, wala hakiwaleweshi. [47]
Na watakuwa nao wanawake wenye macho ya staha mazuri. [48]
Hao wanawake kama mayai yaliyo hifadhika. [49]
Waingie kuulizana wenyewe kwa wenyewe. [50]
Aseme msemaji mmoja miongoni mwao: Hakika mimi nalikuwa na rafiki. [51]
Aliye kuwa akinambia: Hivyo wewe ni katika wanao sadiki. [52]
Ati tukisha kufa tukawa udongo na mafupa, ndio tutalipwa na kuhisabiwa? [53]
Atasema: Je! Nyie mnawaona? [54]
Basi atachungulia amwone katikati ya Jahannamu. [55]
Atasema: Wallahi! Ulikaribia kunipoteza. [56]
Na lau kuwa si neema ya Mola wangu Mlezi bila ya shaka ningeli kuwa miongoni mwa walio hudhurishwa. [57]
Je! Sisi hatutakufa, [58]
Isipo kuwa kifo chetu cha kwanza? Wala sisi hatutaadhibiwa. [59]
Hakika huku bila ya shaka ndiko kufuzu kukubwa. [60]
Kwa mfano wa haya nawatende watendao. [61]
Je! Kukaribishwa hivi si ndio bora, au mti wa Zaqqum? [62]
Hakika Sisi tumeufanya huo kuwa ni mateso kwa walio dhulumu. [63]
Hakika huo ni mti unao toka katikati ya Jahannamu. [64]
Mashada ya matunda yake kama kwamba vichwa vya mashet'ani. [65]
Basi hakika bila ya shaka hao watayala hayo, na wajaze matumbo. [66]
Kisha juu yake wanyweshwe mchanganyo wa maji yamoto yaliyo chemka. [67]
Kisha hakika marejeo yao bila ya shaka yatakuwa kwenye Jahannamu. [68]
Hakika waliwakuta baba zao wamepotea. [69]
Na wao wakafanya haraka kufuata nyayo zao. [70]
Na wao wakafanya haraka kufuata nyayo zao. [71]
Na Sisi hakika tuliwapelekea waonyaji. [72]
Basi hebu angalia ulikuje mwisho wa walioonywa. [73]
Isipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu waliokhitariwa. [74]
Na hakika Nuhu alitwita, na Sisi ni bora wa waitikiaji. [75]
Na tulimwokoa yeye na ahali zake kutokana na msiba mkubwa. [76]
Na tuliwajaalia dhuriya zake ndio wenye kubakia. [77]
Na tukamwachia (sifa njema) kwa walio kuja baadaye. [78]
Iwe salama kwa Nuhu ulimwenguni kote! [79]
Kwa hakika hivi ndivyo tunavyo walipa wanao fanya mema. [80]
Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini. [81]
Kisha tukawazamisha wale wengine. [82]
Na hakika Ibrahim alikuwa katika kundi lake, [83]
Alipo mjia Mola wake Mlezi kwa moyo mzima. [84]
Alimwambia baba yake na watu wake: Mnaabudu nini? [85]
Kwa kuzua tu mnataka miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu? [86]
Mnamdhania nini Mola Mlezi wa walimwengu wote? [87]
Kisha akapiga jicho kutazama nyota. [88]
Akasema: Hakika mimi ni mgonjwa! [89]
Nao wakamwacha, wakampa kisogo. [90]
Basi akaiendea miungu yao kwa siri, akaiambia: Mbona hamli? [91]
Mna nini hata hamsemi? [92]
Kisha akaigeukia kuipiga kwa mkono wa kulia. [93]
Basi wakamjia upesi upesi. [94]
Akasema: Hivyo mnaviabudu vitu mnavyo vichonga wenyewe [95]
Na hali Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni nyinyi na hivyo mnavyo vifanya! [96]
Wakasema: Mjengeeni jengo, na kisha mtupeni motoni humo! [97]
Basi walitaka kumfanyia vitimbi, lakini tukawafanya wao ndio wa chini. [98]
Na akasema: Hakika mimi nahama, nakwenda kwa Mola wangu Mlezi; Yeye ataniongoa. [99]
Ewe Mola wangu Mlezi! Nitunukie aliye miongoni mwa watenda mema. [100]
Basi tukambashiria mwana aliye mpole. [101]
Basi alipo fika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia wewe, waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyo amrishwa, utanikuta mimi, Inshallah, katika wanao subiri. [102]
Basi wote wawili walipo jisalimisha, na akamlaza juu ya kipaji. [103]
Tulimwita: Ewe Ibrahim!. [104]
Umekwisha itimiliza ndoto. Hakika hivi ndivyo tunavyo walipa wanao tenda mema. [105]
Hakika haya ni majaribio yaliyo dhaahiri. [106]
Basi tukamtolea fidia kwa dhabihu mtukufu. [107]
Na tukamwachia (sifa njema) kwa watu walio kuja baadaye. [108]
Iwe salama kwa Ibrahim!. [109]
Hivi ndivyo tunavyo walipa wanao fanya mema. [110]
Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini. [111]
Na tukambashiria kuzaliwa Is-haqa, naye ni Nabii miongoni mwa watu wema. [112]
Na tukambarikia yeye na Is-haqa. Na miongoni mwa dhuriya zao walitokea wema na wenye kudhulumu nafsi zao waziwazi. [113]
Na kwa hakika tuliwafanyia hisani Musa na Haruni. [114]
Na tukawaokoa wao na watu wao kutokana na dhiki kubwa. [115]
Na tukawanusuru; na wakawa wao ndio wenye kushinda. [116]
Na tukawapa wawili hao Kitabu kinacho bainisha. [117]
Na tukawaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka. [118]
Na tukawaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka. [119]
Iwe salama kwa Musa na Haruni!. [120]
Hakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema. [121]
Hakika wawili hao ni katika waja wetu walio amini. [122]
Na hakika Ilyas bila ya shaka alikuwa miongoni mwa Mitume. [123]
Alipo waambia watu wake: Hamwogopi?. [124]
Mnamwomba Baa'li na mnamwacha Mbora wa waumbaji,. [125]
Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa zamani?. [126]
Wakamkadhibisha. Basi kwa hakika watahudhurishwa;. [127]
Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa. [128]
Na tumemwachia (sifa nzuri) kwa walio kuja baadaye. [129]
Iwe salama kwa Ilyas. [130]
Hakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema. [131]
Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini. [132]
Na hakika Lut'i bila ya shaka ni miongoni mwa Mitume. [133]
Tulipo mwokoa yeye na ahali zake wote,. [134]
Isipo kuwa mwanamke mkongwe katika wale walio bakia nyuma. [135]
Kisha tukawaangamiza wale wengineo. [136]
Na hakika nyinyi mnawapitia wakati wa asubuhi,. [137]
Na usiku. Basi je! Hamyatii akilini?. [138]
Na hakika Yunus alikuwa miongoni mwa Mitume. [139]
Alipo kimbia katika jahazi lilio sheheni. [140]
Akaingia katika kupigiwa kura, na akawa katika walio shindwa. [141]
Samaki akammeza hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa. [142]
Na ingeli kuwa hakuwa katika wanao mtakasa Mwenyezi Mungu,. [143]
Bila ya shaka angeli kaa ndani yake mpaka siku ya kufufuliwa. [144]
Lakini tulimtupa ufukweni patupu, hali yu mgonjwa. [145]
Na tukauotesha juu yake mmea wa kabila ya mung'unye. [146]
Na tulimtuma kwa watu laki moja au zaidi. [147]
Basi wakaamini, na tukawastarehesha kwa muda. [148]
Basi waulize: Ati Mola wako Mlezi ndiye mwenye watoto wa kike, na wao wanao watoto wa kiume?. [149]
Au tumewaumba Malaika kuwa ni wanawake, na wao wakashuhudia?. [150]
Ati ni kwa uzushi wao ndio wanasema:. [151]
Mwenyezi Mungu amezaa! Ama hakika bila ya shaka hao ni waongo!. [152]
Ati amekhiari watoto wa kike kuliko wanaume?. [153]
Mna nini? Mnahukumu vipi nyinyi?. [154]
Hamkumbuki?. [155]
Au mnayo hoja iliyo wazi?. [156]
Basi leteni Kitabu chenu kama mnasema kweli. [157]
Na wameweka makhusiano ya nasaba baina yake na majini; na majini wamekwisha jua bila ya shaka kuwa wao watahudhurishwa. [158]
Subhana 'Llah Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo msingizia. [159]
Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa. [160]
Basi hakika nyinyi na mnao waabudu. [161]
Hamwezi kuwapoteza. [162]
Isipo kuwa yule atakaye ingia Motoni. [163]
Na hapana katika sisi ila anapo mahali pake maalumu. [164]
Na hakika bila ya shaka sisi ndio wajipangao safu. [165]
Na hakika sisi ndio wenye kusabihi kutakasa. [166]
Na walikuwapo walio kuwa wakisema:. [167]
Tungeli kuwa na Ukumbusho kama wa watu wa zamani,. [168]
Bila ya shaka tungeli kuwa ni waja wa Mwenyezi Mungu wenye ikhlasi. [169]
Lakini waliukataa. Basi watakuja jua. [170]
Na bila ya shaka neno letu lilikwisha tangulia kwa waja wetu walio tumwa. [171]
Ya kuwa wao bila ya shaka ndio watakao nusuriwa. [172]
Na kwamba jeshi letu ndilo litakalo shinda. [173]
Basi waachilie mbali kwa mda. [174]
Na watazame, nao wataona. [175]
Je! Wanaihimiza adhabu yetu?. [176]
Basi itakapo shuka uwanjani kwao, itakuwa asubuhi mbaya kwa walio onywa. [177]
Na waache kwa muda. [178]
Na tazama, na wao wataona. [179]
Subhana Rabbi'l'Izzat Ametakasika Mola Mlezi Mwenye enzi na yale wanayo mzulia. [180]
Na Salamu juu ya Mitume. [181]
Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote. [182]