عربيEnglish

The Noble Qur'an Encyclopedia

Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languages

Sad [Sad] - Swahili translation - Ali Muhsen Al-Berwani

Surah Sad [Sad] Ayah 88 Location Maccah Number 38

Mataifa mangapi tumeyaangamiza kabla yao, na wakapiga kelele, lakini wakati wa kuokoka ulikwisha pita. [3]

Ati yeye tu ndiye aliye teremshiwa mawaidha peke yake katika sisi? Lakini hao wana shaka na mawaidha yangu, bali hawajaionja adhabu yangu. [8]

Hao ni askari watao shindwa miongoni mwa makundi yatayo shindwa. [11]

Hao wote waliwakadhibisha Mitume; basi wakastahiki adhabu yangu. [14]

Na wao husema: Mola wetu Mlezi! Tuletee upesi sehemu yetu ya adhabu kabla ya Siku ya Hisabu. [16]

Na pia ndege walio kusanywa makundi kwa makundi; wote walikuwa wanyenyekevu kwake. [19]

Na tukayafanya mashet'ani yamtumikie, wote wajenzi na wapiga mbizi. [37]

Na hakika yeye kwetu Sisi ana cheo cha kukaribishwa kwetu, na pahala pazuri pa kurejea. [40]

(Akaambiwa:) Piga-piga ardhi kwa mguu wako! Basi haya maji baridi ya kuogea na ya kunywa. [42]

Na shika kicha cha vijiti tu mkononi mwako, kisha ndio upigie nacho, wala usivunje kiapo. Hakika tulimkuta mwenye subira, mbora wa waja, kwa hakika alikuwa mwingi wa kutubu. [44]

Ndio hivi! Na hakika wenye kuasi bila ya shaka watapata marudio maovu kabisa; [55]

Nayo ni Jahannamu! Wataingia humo. Nacho hicho ni kitanda kiovu mno cha kulalia. [56]

Ndio hivi! Basi na wayaonje maji ya moto na ya usaha! [57]

Hakika hayo bila ya shaka ndiyo makhasimiano ya watu wa Motoni. [64]

Sema: Hii ni khabari kubwa kabisa. [67]

Mwenyezi Mungu akamwambia: Ewe Iblisi! Kipi kilicho kuzuia kumt'ii yule niliye muumba kwa mikono yangu? Je! Umejiona mkubwa, au umekuwa katika wakuu kweli? [75]

Akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe umelaanika. [77]

Akasema: Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka siku watayo fufuliwa viumbe. [79]

Mwenyezi Mungu akasema: Basi umekwisha kuwa miongoni mwa walio pewa muhula, [80]

Akasema (Iblisi): Naapa kwa utukufu wako, bila ya shaka nitawapoteza wote, [82]

Isipo kuwa wale waja wako miongoni mwao walio khitariwa. [83]

Bila ya shaka nitaijaza Jahannamu kwa wewe na kwa hao wote wenye kukufuata miongoni mwao. [85]

Hayakuwa haya ila ni mawaidha kwa walimwengu wote. [87]

Na bila ya shaka mtajua khabari zake baada ya muda. [88]