The Noble Qur'an Encyclopedia
Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languagesThe emissaries [Al-Mursalat] - Swahili translation - Ali Muhsen Al-Berwani
Surah The emissaries [Al-Mursalat] Ayah 50 Location Maccah Number 77
Naapa kwa zinazo tumwa kwa upole! [1]
Na zinazo vuma kwa kasi! [2]
Na zikaeneza maeneo yote! [3]
Na zinazo farikisha zikatawanya! [4]
Na zinazo peleka mawaidha! [5]
Kwa kuudhuru au kuonya, [6]
Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka yatakuwa! [7]
Wakati nyota zitakapo futwa, [8]
Na mbingu zitakapo pasuliwa, [9]
Na milima itakapo peperushwa, [10]
Na Mitume watakapo wekewa wakati wao, [11]
Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo? [12]
Kwa siku ya kupambanua! [13]
Na nini kitakacho kujuulisha siku ya kupambanua ni nini? [14]
Ole wao, siku hiyo hao wanao kanusha! [15]
Kwani hatukuwaangamiza walio tangulia? [16]
Kisha tukawafuatilizia walio fuatia? [17]
Ndio kama hivi tuwatendavyo wakosefu! [18]
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! [19]
Kwani hatukukuumbeni kwa maji ya kudharauliwa? [20]
Kisha tukayaweka mahali pa utulivu madhubuti? [21]
Mpaka muda maalumu? [22]
Tukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria. [23]
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! [24]
Kwani hatukuifanya ardhi yenye kukusanya [25]
Walio hai na maiti? [26]
Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, na tunakunywesheni maji matamu? [27]
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! [28]
Nendeni kwenye adhabu mliyo kuwa mkiikanusha! [29]
Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu! [30]
Hakikingi moto, wala hakiwaepushi na mwako. [31]
Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba! [32]
Kama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano! [33]
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! [34]
Hii ni siku ambayo hawatatamka kitu, [35]
Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru. [36]
Ole wao siku hiyo hao walio kanusha! [37]
Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na walio tangulia. [38]
kiwa mnayo hila, nifanyieni hila Mimi! [39]
Ole wao siku hiyo hao walio kanusha! [40]
Hakika wachamngu watakuwa katika vivuli na chemchem, [41]
Na matunda wanayo yapenda, [42]
Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda. [43]
Hakika ndio kama hivyo tunavyo walipa watendao mema. [44]
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! [45]
Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni wakosefu! [46]
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! [47]
Na wakiambiwa: Inameni! Hawainami. [48]
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! [49]
Basi maneno gani baada ya haya watayaamini? [50]