The Noble Qur'an Encyclopedia
Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languagesThe tidings [An-Naba] - Swahili translation - Ali Muhsen Al-Berwani
Surah The tidings [An-Naba] Ayah 40 Location Maccah Number 78
WANAULIZANA nini? [1]
Ile khabari kuu! [2]
Ambayo kwayo wanakhitalifiana. [3]
La! Karibu watakuja jua. [4]
Tena la! Karibu watakuja jua. [5]
kaKwani hatukuifanya ardhi ma tandiko? [6]
kama Na milima vigingi? [7]
Na tukakuumbeni kwa jozi? [8]
Na tukakufanya kulala kwenu ni mapumziko? [9]
Na tukaufanya usiku ni nguo? [10]
Na tukaufanya mchana ni wa kuchumia maisha? [11]
Na tukajenga juu yenu saba zenye nguvu? [12]
Na tukaifanya taa yenye mwanga na joto; [13]
Na tukateremsha maji yanayo anguka kwa kasi kutoka mawinguni, [14]
Ili tutoe kwayo nafaka na mimea. [15]
Na mabustani yenye miti iliyo kamatana. [16]
Hakika siku ya uamuzi imewekewa wakati wake, [17]
Siku litapo pulizwa barugumu, nanyi mtakuja kwa makundi, [18]
Na mbingu zitafunguliwa, ziwe milango. [19]
Na milima itaondolewa na itakuwa kama sarabi. [20]
Hakika Jahannamu inangojea! [21]
Kwa walio asi ndio makaazi yao, [22]
Wakae humo karne baada ya karne, [23]
Hawataonja humo chochote kibaridi wala kinywaji, [24]
Ila maji yamoto sana na usaha, [25]
Ndio jaza muwafaka. [26]
Hakika hao hawakuwa wakitaraji kuwa kuna hisabu. [27]
Na wakikanusha Aya zetu kwa nguvu. [28]
Na kila kitu Sisi tumekidhibiti kwa kukiandika. [29]
Basi onjeni! Nasi hatutakuzidishieni ila adhabu! [30]
Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu, [31]
Mabustani na mizabibu, [32]
Na wake walio lingana nao, [33]
Na bilauri zilizo jaa, [34]
Hawatasikia humo upuuzi wala uwongo, [35]
Malipo kutoka kwa Mola wako Mlezi, kipawa cha kutosha. [36]
Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, Arrahman, Mwingi wa rehema; hawamiliki usemi mbele yake! [37]
Siku atakapo simama Roho na Malaika kwa safu. Hawatasema ila Mwingi wa rehema aliye mruhusu, na atasema yaliyo sawa tu. [38]
Hiyo ndiyo Siku ya haki. Basi anaye taka na ashike njia arejee kwa Mola wake Mlezi [39]
Hakika tumekuhadharisheni adhabu iliyo karibu kufika; Siku ambayo mtu atakapo ona yaliyo tangulizwa na mikono yake; na kafiri atasema: Laiti ningeli kuwa udongo! [40]