The Noble Qur'an Encyclopedia
Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languagesThose who drag forth [An-Naziat] - Swahili translation - Ali Muhsen Al-Berwani
Surah Those who drag forth [An-Naziat] Ayah 46 Location Maccah Number 79
Naapa kwa wanao komoa kwa nguvu! [1]
Na kwa wanao toa kwa upole! [2]
Na wanao ogelea! [3]
Wakishindana mbio! [4]
Wakidabiri mambo. [5]
Siku kitapo tetemeka cha kutetemeka! [6]
Kifuate cha kufuatia. [7]
Siku hiyo nyoyo zitapiga piga! [8]
Macho yatainama chini! [9]
Sasa wanasema: Ati kweli tutarudishwa kwenye hali ya kwanza? [10]
Hata tukiwa mifupa iliyo bunguliwa? [11]
Wanasema: Basi marejeo hayo ni yenye khasara! [12]
Kwa hakika hayo ni ukelele mmoja tu, [13]
Mara watakuwa kwenye uwanda wa mkutano! [14]
Je! Imekufikia hadithi ya Musa? [15]
Mola wake Mlezi alipo mwita katika bonde takatifu la T'uwaa, akamwambia: [16]
Nenda kwa Firauni. Hakika yeye amezidi jeuri [17]
Umwambie: Je! Unapenda kujitakasa? [18]
Nami nitakuongoa ufike kwa Mola wako Mlezi, upate kumcha. [19]
Basi alimwonyesha Ishara kubwa. [20]
Lakini aliikadhibisha na akaasi. [21]
Kisha alirudi nyuma, akaingia kufanya juhudi. [22]
Akakusanya watu akanadi. [23]
Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi mkuu kabisa. [24]
Basi hapo Mwenyezi Mungu akamshika kumuadhibu kwa la mwisho na la mwanzo. [25]
Kwa hakika katika haya yapo mazingatio kwa wanao ogopa. [26]
Je! Ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu? Yeye ndiye aliye ijenga! [27]
Akainua kimo chake, na akaitengeneza vizuri. [28]
Na akautia giza usiku wake, na akautokeza mchana wake [29]
Na juu ya hivyo ameitandaza ardhi. [30]
Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake, [31]
Na milima akaisimamisha, [32]
Kwa nafuu yenu na mifugo yenu. [33]
Basi itakapo fika hiyo balaa kubwa, [34]
Siku ambayo mtu atakumbuka aliyo yafanya, [35]
Na Jahannamu itadhihirishwa kwa mwenye kuona, [36]
Basi ama yule aliye zidi ujeuri, [37]
Na akakhiari maisha ya dunia, [38]
Kwa hakika Jahannamu ndiyo makaazi yake! [39]
Na ama yule anaye ogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi, na akajizuilia nafsi yake na matamanio, [40]
Basi huyo, Pepo itakuwa ndiyo makaazi yake! [41]
Wanakuuliza Saa (ya Kiyama) itakuwa lini? [42]
Una nini wewe hata uitaje? [43]
Kwa Mola wako Mlezi ndio mwisho wake. [44]
Kwa hakika wewe ni mwonyaji tu kwa mwenye kuikhofu. [45]
Ni kama kwamba wao siku watapo iona (hiyo Saa) hawakukaa ila jioni moja tu, au mchana wake. [46]