The Noble Qur'an Encyclopedia
Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languagesThe Cleaving [AL-Infitar] - Swahili translation - Ali Muhsen Al-Berwani
Surah The Cleaving [AL-Infitar] Ayah 19 Location Maccah Number 82
Mbingu itapo chanika! [1]
Na nyota zitapo tawanyika! [2]
Na bahari zitakapo pasuliwa! [3]
Na makaburi yatapo fukuliwa! [4]
Hapo kila nafsi itajua ilicho tanguliza, na ilicho bakisha nyuma. [5]
Ewe mwanaadamu! Nini kilicho kughuri ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu? [6]
Aliye kuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha! [7]
Katika sura yoyote aliyo ipenda akakujenga. [8]
Sivyo hivyo! Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Malipo. [9]
Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu, [10]
Waandishi wenye hishima, [11]
Wanayajua mnayo yatenda. [12]
Hakika wema bila ya shaka watakuwa katika neema, [13]
Na hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni; [14]
Wataingia humo Siku ya Malipo. [15]
Na hawatoacha kuwamo humo. [16]
Na nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani? [17]
Tena nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani? [18]
Siku ambayo nafsi haitakuwa na madaraka yoyote juu ya nafsi; na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu. [19]