The Noble Qur'an Encyclopedia
Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languagesThe morning star [At-Tariq] - Swahili translation - Ali Muhsen Al-Berwani
Surah The morning star [At-Tariq] Ayah 17 Location Maccah Number 86
Naapa kwa mbingu na Kinacho kuja usiku! [1]
Na nini kitakacho kujuulisha ni nini hicho Kinacho kuja usiku? [2]
Ni Nyota yenye mwanga mkali. [3]
Hapana nafsi ila inayo mwangalizi. [4]
Hebu naajitazame mwanaadamu ameumbwa kwa kitu gani? [5]
Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa! [6]
Yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu. [7]
Hakika Yeye ana uweza wa kumrudisha. [8]
Siku zitakapo dhihirishwa siri. [9]
Basi hatakuwa na nguvu wala msaidizi. [10]
Naapa kwa mbingu yenye marejeo! [11]
Na kwa ardhi inayo pasuka! [12]
Hakika hii ni kauli ya kupambanua. [13]
Wala si mzaha. [14]
Hakika wao wanapanga mpango. [15]
Na Mimi napanga mpango. [16]
Basi wape muhula makafiri - wape muhula pole pole. [17]