The Noble Qur'an Encyclopedia
Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languagesThe Most High [Al-Ala] - Swahili translation - Ali Muhsen Al-Berwani
Surah The Most High [Al-Ala] Ayah 19 Location Maccah Number 87
Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa! [1]
Aliye umba, na akaweka sawa! [2]
Na ambaye amekadiria na akaongoa,. [3]
Na aliye otesha malisho! [4]
Kisha akayafanya makavu, meusi. [5]
Tutakusomesha wala hutasahau! [6]
Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahiri na yaliyo fichikana. [7]
Na tutakusahilishia yawe mepesi. [8]
Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa. [9]
Atakumbuka mwenye kuogopa. [10]
Na atajitenga mbali nayo mpotovu, [11]
Ambaye atauingia Moto mkubwa. [12]
Tena humo hatakufa wala hawi hai. [13]
Hakika amekwisha fanikiwa aliye jitakasa. [14]
Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akaswali. [15]
Lakini nyinyi mnakhiari maisha ya dunia! [16]
Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi. [17]
Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo, [18]
Vitabu vya Ibrahimu na Musa. [19]