The Noble Qur'an Encyclopedia
Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languagesThe Overwhelming [Al-Ghashiya] - Swahili translation - Ali Muhsen Al-Berwani
Surah The Overwhelming [Al-Ghashiya] Ayah 26 Location Maccah Number 88
Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza? [1]
Siku hiyo nyuso zitainama! [2]
Zikifanya kazi, nazo taabani. [3]
Ziingie katika Moto unao waka . [4]
Zikinyweshwa kutoka chemchem inayo chemka. [5]
Hawatakuwa na chakula isipo kuwa kichungu chenye miba. [6]
Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa. [7]
Siku hiyo nyuso nyengine zitakuwa kunjufu. [8]
Zitakuwa radhi kwa juhudi yao! [9]
Katika Bustani ya juu. [10]
Hawatasikia humo upuuzi.Humo imo chemchem inayo miminika. [11]
Humo imo chemchem inayo miminika. [12]
Humo vimo viti vilivyo nyanyuliwa, [13]
Na bilauri zilizo pangwa, [14]
Na matakia safu safu, [15]
Na mazulia yaliyo tandikwa. [16]
Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa? [17]
Na mbingu jinsi ilivyo inuliwa? [18]
Na milima jinsi ilivyo thibitishwa? [19]
Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa? [20]
Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji. [21]
Wewe si mwenye kuwatawalia. [22]
Lakini anaye rudi nyuma na kukataa, [23]
Basi Mwenyezi Mungu atamuadhibu kwa adhabu iliyo kubwa kabisa! [24]
Hakika ni kwetu Sisi ndio marejeo yao. [25]
Kisha hakika ni juu yetu Sisi hisabu yao! [26]