The Noble Qur'an Encyclopedia
Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languagesThe City [Al-Balad] - Swahili translation - Ali Muhsen Al-Berwani
Surah The City [Al-Balad] Ayah 20 Location Maccah Number 90
Naapa kwa Mji huu! [1]
Nawe unaukaa Mji huu. [2]
Na naapa kwa mzazi na alicho kizaa. [3]
Hakika tumemuumba mtu katika taabu. [4]
Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza? [5]
Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali. [6]
Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona? [7]
Kwani hatukumpa macho mawili? [8]
Na ulimi, na midomo miwili? [9]
Na tukambainishia zote njia mbili? [10]
Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani. [11]
Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani? [12]
Kumkomboa mtumwa; [13]
Au kumlisha siku ya njaa [14]
Yatima aliye jamaa, [15]
Au masikini aliye vumbini. [16]
Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana. [17]
Hao ndio watu wa kheri wa kuliani. [18]
Lakini walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni. [19]
Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande. [20]