The Noble Qur'an Encyclopedia
Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languagesThe Sun [Ash-Shams] - Swahili translation - Ali Muhsen Al-Berwani
Surah The Sun [Ash-Shams] Ayah 15 Location Maccah Number 91
Naapa kwa jua na mwangaza wake! [1]
Na kwa mwezi unapo lifuatia! [2]
Na kwa mchana unapo lidhihirisha! [3]
Na kwa usiku unapo lifunika! [4]
Na kwa mbingu na kwa aliye ijenga! [5]
Na kwa ardhi na kwa aliye itandaza! [6]
Na kwa nafsi na kwa aliye itengeneza! [7]
Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake! [8]
Hakika amefanikiwa aliye itakasa! [9]
Na hakika amekhasiri aliye iviza. [10]
Kina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotofu wao, [11]
Alipo simama mwovu wao mkubwa, [12]
Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipo waambia: Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, mwacheni anywe maji fungu lake. [13]
Lakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa. [14]
Wala Yeye haogopi matokeo yake. [15]