The Noble Qur'an Encyclopedia
Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languagesThe night [Al-Lail] - Swahili translation - Ali Muhsen Al-Berwani
Surah The night [Al-Lail] Ayah 21 Location Maccah Number 92
Naapa kwa usiku unapo funika! [1]
Na mchana unapo dhihiri! [2]
Na kwa Aliye umba dume na jike! [3]
Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali. [4]
Ama mwenye kutoa na akamchamngu! [5]
Na akaliwafiki lilio jema! [6]
Tutamsahilishia yawe mepesi. [7]
Na ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na haja ya wenzake! [8]
Na akakanusha lilio jema! [9]
Tutamsahilishia yawe mazito! [10]
Na mali yake yatamfaa nini atapo kuwa anadidimia? [11]
Hakika ni juu yetu kuonyesha uwongofu. [12]
Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia. [13]
Basi nakuonyeni na Moto unao waka! [14]
Hatauingia ila mwovu kabisa! [15]
Anaye kadhibisha na kupa mgongo. [16]
Na mchamngu ataepushwa nao, [17]
Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa. [18]
Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliye mfanyia hisani ndio anamlipa. [19]
Ila ni kutaka radhi ya Mola wake Mlezi aliye juu kabisa. [20]
Naye atakuja ridhika! [21]