The Noble Qur'an Encyclopedia
Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languagesThe morning hours [Ad-Dhuha] - Swahili translation - Ali Muhsen Al-Berwani
Surah The morning hours [Ad-Dhuha] Ayah 11 Location Maccah Number 93
Naapa kwa mchana! [1]
Na kwa usiku unapo tanda! [2]
Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe. [3]
Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia. [4]
Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike. [5]
Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi? [6]
Na akakukuta umepotea akakuongoa? [7]
Akakukuta mhitaji akakutosheleza? [8]
Basi yatima usimwonee! [9]
Na anaye omba au kuuliza usimkaripie! [10]
Na neema za Mola wako Mlezi zisimlie. [11]