The Noble Qur'an Encyclopedia
Towards providing reliable exegeses and translations of the meanings of the Noble Qur'an in the world languagesThe Clot [Al-Alaq] - Swahili translation - Ali Muhsen Al-Berwani
Surah The Clot [Al-Alaq] Ayah 19 Location Maccah Number 96
Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba! [1]
Amemuumba binaadamu kwa tone la damu! [2]
Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! [3]
Ambaye amefundisha kwa kalamu. [4]
Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui. [5]
Kwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri. [6]
Akijiona katajirika. [7]
Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo. [8]
Umemwona yule anaye mkataza. [9]
Mja anapo sali? [10]
Umeona kama yeye yuko juu ya uwongofu? [11]
Au anaamrisha uchamngu? [12]
Umeona kama yeye akikanusha na anarudi nyuma? [13]
Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona? [14]
Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele! [15]
Shungi la uwongo, lenye makosa! [16]
Basi na awaite wenzake! [17]
Nasi tutawaita Mazabania! [18]
Hasha! Usimt'ii! Nawe sujudu na ujongee! [19]